JUMA LA TATU
Mtazamo—Picha Thabiti
Mwongozo: Ulimwengu Kama Unavyopaswa Kuwa


Baada ya majuma mawili ya kupitia na kutafakari hadithi ya maisha yetu na kuiona kama hadithi ya uwepo wa Mungu asiyetutelekeza kamwe, sasa tunasonga mbele kuwa na mtazamo mpana zaidi.

Katika juma hili tunanataka kutafakari juu ya ufunuo wa nia ya Mungu kutuumba sisi na viumbe vingine vyote.
Mtakatifu Inyasi wa Loyola kautafsiri ufunuo wa nia ya Mungu kwa maneno machache:

 


Mungu katuumba kumsifu, kumtukuza na kumtumikia yeye
na katika kutakeleza hayo, sisi kupata wokovu wa roho zetu.
Mungu kaumba viumbe vingine vyote
kututusaidia kutekeleza nia hiyo ya kuumbwa kwetu naye Mungu

Katika juma hili tuweke moyoni na kutilia maanani tafakari mbili nzuri:

  • Ninapokuwa nikifanya kazi zangu za kawaida na kuendelea na shunguli zingine za kila siku, nijitahidi kuwa daima kutanabahi au kuwa na utambuzi wa nia ya Mungu kuniumba mimi:

Kumsifu Mungu.

Kumsimtukuza Mungu: kukua katika kumhimidi na kumpenda Mungu
Kutumikia: kuwa katika utumishi wa Mungu.

  • Kuwa makini zaidi katika kutambua uwepo wa viumbe vingine na nia ya Mungu ya kuviumba vyote hivyo kunisaidia mimi — vyote vimeumbwa kwa ajili yangu.

Lengo la tafakari hii ni kuwa na shukrani.  Tunataka kuthamini, kujali zaidi na kuwa na utambuzi mahususi wa jambo fulani limhusulo Mungu Muumba wetu:  Hivyo basi kwa kutazama na kuwaza kwetu katika juma hili, tunategemea kumjua Mungu vema zaidi.

Tumia vema miongozo unayopewa juma hili.  Tuipe nafasi picha hii kubwa (ambayo ina Mungu Muumba, sisi viumbe vyake wapendwa na viumbe vingine) ituvutie tumstaajabie Mungu, tumhimidi na kuwa na elimu ya mpango wa wake kwa ajili ya maisha yetu.  Katika juma hili, tujaribu kuanza na kumalizia kila siku kuweka wazi kupokea na kufurahia sana yote ambayo Mungu anataka kutufunulia.


Zana za Kukusaidia Kuanza Juma Hili

Katika juma hili la tatu, mtazamo wetu unabadilika.  Tazama jinsi picha ya wiki hii ilivyo na upana wa kustaajabisha na utaona jinsi ya kulianza juma hili.

Kuhusu mtazamo: katika juma hili tutajaribu kujiweka pembeni, na kujiona sisi kati ya viumbe vyote.  Hivyo, katika juma hili lote, upe nafasi ulimwengu wa mtazamo wetu ukue kuifikia picha hii iliyopanuka kuhusisha uumbaji wote wa Mungu.  Hata hivyo usiache picha hiyo iwe kubwa kupita kiasi kukufanya ushindwe kuitafakari.

Kuhusu lengo, kuwa na mwelekeo madhubuti kunaweza kutusaidia sana.  Katika juma zima, fikiria ni kwa sababu gani viumbe hai na visivyo hai vipo.  Hili lisiwe zoezi gumu sana, anza na urahisi kama utambuzi wa sababu ya kuweko kwa sufuria, chai katika kikombe chako, mahindi, unga, karatasi, simu, ng’ombe, majani, maji, jua nk.  Unapoona, unapohisi, unaposikia, unapofikiria, unaponusa au kupata ladha ya chochote jaribu kuwa na utambuzi wa sababu ya kitu hicho kuwepo katika maisha yako.  Taratibu utaanza uona ukweli wa maneno ya Mtakatifu Inyasi.  Vyote vimeumbwa kwa nia madhubuti na wala haviko kwa bahati nasibu.  Viumbe vimeumbwa ili viwe vya msaada fulani kwangu — vimeumbwa kunisaidia kuiishi au kuitekeleza nia ya kuumbwa kwangu.

Usisahau zoezi tunalofanya ni kwa ajili ya kutusaidia kuwa na uwezo zaidi wa kutafuta, kuona, kushuhudia kile kituunganishacho na Mungu katika vyote tunavyokutana navyo katika shughuli zetu za kila siku.  Ndiyo maana katika juma hili tunajitahidi kutambua uwepo wa vitu vingi ndani ya maisha yetu na kuzunguka maisha yetu, na tunafanya makusudi ya kutembea na swali linalohoji sababu ya kuwepo kwa kila kitu tunachokutana nacho.  Kwa msaada, najaribu kufanya zoezi la kutafakari sababu — kwa mfano ninapoelekea mkutanoni, au ninapoelekea kwenye meza palipotengwa chakula, au ninapoenda hospitali — naamua kutafakari sababu ya kwenda huko, na sababu hii siwezi kuitaja bila kuhusisha vitu vingine vinavyonisaidia kwenda huko na kutenda ninalotazamia kutenda.  Nikifanya mazoezi kama hili mara kwa mara, naweza kujipa nafasi nyingi fupi fupi za kuwa na mtazamo wa picha kubwa ya mimi katika ya viumbe vingine vya Mungu; nitajiona kuwa nimeumbwa, kama sehemu ya viumbe anuwai vya Mungu, kwa nia ya kumsifu, kumtukuza na kumtumikia Mungu Mkuu.

Kumbuka pia dhana nyingine za kufanya mafungo haya ulizopewa katika majuma yaliyopita.  Kutambua neema ulizopewa ni muhimu sana, na kutoa shukrani kwa neema hizo si jambo la kutotilia maanani wala kusahau.  Jaribu kujiuliza: ni lipi ninalopokea juma hili?  Jaribu kusema “Asante sana Mungu kwa kunifunulia picha hiyo kubwa inayoonyesha nafasi yangu mbele zako na baina ya viumbe vyako vingi.”  “Mungu asante kwa kunikumbusha kuwa umeniumba kwa sababu maalum.”

Kumbuka kuwa miili yetu ina nafasi ya pekee katika kutafakari.  Ni mkao gani ambao unanisaidia kuelezea kinaganaga nitakalo? Kwa mfano naweza naweza kujidhani nimesimama na naiangalia picha ya viumbe vyote vya Mungu na mimi nikiwa nimechukua nafasi yangu katika picha hiyo — katika kustaajabia na kumshukuru Mungu kwa uumbaji wake naweza kunyanyua mikono yangu juu nikimsifu Mungu Muumba.  Kwa namna hiyo, kabla ya kulala usiku au mara baada ya kuamka asubuhi, nikinyanya mikono yangu juu kwa kumsiufu Muumba, tafakari yote ya viumbe vyake na mimi nikiwa na nafasi maalum kati ya viumbe hivyo inanijia na kitendo kifupi cha kunyanyua mikono juu kinakuwa sala kubwa ya kumsifu Mungu Muumba inayoendelea.  Hii yaweza pia kutokea kwamba nikajikuta navutiwa kumpigia Mungu magoti kwa kumtukuza na kumhimidi nikiwa baina ya viumbe wake.  Naweza pia kuketi katika kiti na kutafakari nipo katika kiti ambapo nauona ulimwengu wote wa viumbe vya Mungu na jinsi viumbe mbalimbali vilivyo na maana katika maisha yangu — hapa naweza kujikuta nikifungua mikono juu ya magoti yangu ikiwa alama ya kuwa wazi na tayari kumtumikia katika namna anayotaka.  Ninapoanza kazi kila siku, nikimfungulia Mungu mikono katika meza ya kazi kama nafanya kazi ofisini, juu ya dawati kama mimi ni mwanafunzi au mwanachuo, katika meza ya jikoni kama mimi ni mpishi, katika usukani wa gari iwapo kazi yangu ni udereva nk. nitakuwa nikikubali katika kazi yangu kuwa mtumishi wa Mungu — nikikubali na kutunza moyoni sababu ya kuumbwa kwangu.  Mwili wangu unakuwa chombo kikuu cha sala na mafungo yangu. Mazoezi haya yanachukua wakati mfupi sana wa siku yetu, lakini matunda yake hudumu maisha yetu yote, daima tukikumbushwa nafasi yetu katika picha isiyo kasoro: sisi kama viumbe wa Mungu walioumbwa kwa sababu maalum ambayo tunasaidiwa na viumbe vingine kuitekeleza.

Usisahau kutumia vema masomo na sala; tunaaza sasa kushuhudia awezayo kufanya Mungu iwapo tunajiweka wazi mbele yake, kumwamini na kumtumainia.

Kwa Ajili ya Safari: Msingi

Msingi wa jengo ndipo jengo lianziapo na lishikiliwapo imara.  Katika Mazoezi ya Kiroho, Mtakatifu Inyasi anaanza na tamko ambalo ni kanuni ya msingi ya uwepo wetu.  Ni kanuni rahisi, ila si njepesi kukubalika mara zote—tamko hilo ni: “Binadamu wanaumbwa.”  Kila mmoja wetu anaumbwa kila wakati na neema ya Mungu na mazoezi tunayopata katika kuishi maisha yetu kila siku.

Mojawapo ya mambo magunu kuyapokea katika kukubali kuwa wanaoumbwa ni kutokuwa wakamilifu; tuna mapungufu bayana ya kila namna.  Tuna umri, ukubwa, uwezo, nafsi, vipaji na kadhalika; ila vyote vina mapungufu ya kutokuwa Mungu.  Sisi tu walioumbwa kwa jinsi na namna aliyotaka Mungu Muumba katika upendo wake.  Mtakatifu Inyasi anaanzia pale ambapo tuna hamu ya kupafikia kwa majaliwa ya Mungu.

Kwa nini tunaumbwa ni sehumu muhimu ndani ya tamko hilo la kanuni ya msingi.  Mtakatifu Inyasi alikuwa anajua wazi majibu mengi ambayo binadamu wanaweza kuyatoa kwa ajili ya swali hili la msingi.  Alikuwa tayari kakubali kuwa Mungu yupo, nasi viumbe wake tupo, ila swali kubwa linalofuata baada ya kukubali hayo sharti lijibiwe.  Jinsi alivyoishi maisha yake kulitegemea jinsi alivyojibu swali hilo kuu.  Hata na sisi jinsi tutakavyojibu swali hilo kutaamua jinsi tutakavyoishi.  Kwa Mtakatifu inyasi, majibu kwa swali hilo yalikuwa mepesi, ila haikuwa rahisi kuyaishi.  Katika mapungufu yetu, tunaumbwa kumsifu Mungu kwa kuwa Muumba asiye na mipaka, na kwa kuumba kila mmoja wetu katika mapungufu yetu ambayo wakati mwingine si rahisi kuyakubali.  Tunaumbwa pia kumtumikia huyu Mungu Muumba kwa kutumia na katika vipaji alivyotujalia; pia kwa kutumia na katika mapungufu yaliyo sehemu ya kuumbwa kwetu.  Hakuna kipaji ambacho ni kwa ajili yetu pekee; ila vipaji nilivyojaliwa na Mungu ni zawadi yake, kupitia kwangu, kwa familia ya uumbaji wake.

Kanuni hii ya pili ya msingi ni kuwa ili kumsifu Mungu sharti tuuheshimu uumbaji wake ambao daima una alama za vidole vya Mungu.  Heshima hii ni kumtukuza Mungu katika mipango na kazi zake.  Kumtukuza Mungu hapa ni utambuzi wa uwepo mtakatifu sana wa Mungu katika viumbe vyake vyote.  Changamoto kwa sala zetu ni kupata uhuru wa kuheshimu mapungufu yetu kiasi kwamba katika maisha yetu tuliyopewa kumtumikia Mungu tunashukuru na hatufichi mapungufu hayo, ila tunayaruhusu yawe ya kinabii.


Katika Maneno Haya au Mengine Yanayofanana Nayo...

Bwana Mungu Muumba,

Leo ninapotakari kuhusu ulimwengu unayonizunguka, inaelekea shukrani ni kitu cha kwamza kinachonijia kichwani.  Katika mafungo juma hili, najaribu kwa namna ya unyenyekevu kutazama maisha yangu, na kuona ukweli wa zawadi zako za asili kwangu na katika mazingira yangu.  Nilipotoka nyumbani asubuhi ya leo, sikuweza kujizuia kutazama na kuona mwanga wa jua uliopenya mawingu ya angani.  Mwanga huu ulifanya rangi ambazo siwezi kuzielezea.  Mti katika mbele ya nyumba niishipo umetoa maua mazuri ya kupendeza na nyuki wanakuja kwa wingi kukusanya asali.  Katika bustani yangu ndogo, nyanya zangu bado zinaendelea kukua na kuiva.

Naona vyote hivi kama zawadi kwetu toka kwako; zawadi kwetu, ila nina shaka iwapo kuna wakati wowote nimeziangalia kama zawadi kwangu kutoka kwako.  Nawezaje kuelewa kina cha upendo wako kwangu — kwamba umeumba kila ua na kila nyanya kwa kuniridhisha?  Acha niwe mkweli Mungu wangu, huwa sipati hata muda wa kuwaza vitu kama hivi.  Sioni sababu ya kuangalia, sembuse kutafakari viumbe ambavyo vipo nami daima, vingi vikifanya sehemu ya maisha yangu.

Sasa nipokusalia, nipo macho na makini, navutiwa na msemo katika mwongozo wa sala wa juma hili: “Mungu alivyotuumba kwa mapendo, aliweka pia njia kamilifu ya kutusaidia kutekeleza nia aliyotuumbia.”  Unaweza kweli kuwa na nia yoyote katika maisha yangu?  Unaweza kweli kuwa na nia yoyote kwangu mimi mtu mmoja dhaifu kati ya mabilioni wanafanya makazi katika sayari hii?

Naangalia nje na naona mazingira asili, na ndami pia walipo jamii yangu na marafiki ulionizungushia na nakuambia “asante”.  Nisaidie Bwana wangu kuweza kukutolea shukrani zangu kwa ajili ya maisha yangu na kwa jinsi unavyonijali.  Nisaidie kuitambua hasa nia ambayo kwayo umeniumba.  Niko radhi kufanya maisha yangu njia ya kukutumikia.


Maandiko Matakatiu

Waefeso 1:3–12
Zaburi 138

MAFUNGO YA KIROHO KUPITIA MTANDAO