JUMA LA TANO
Vurugu ya Dhambi—Tishio la Uasi
Mwongozo: Maana ya Dhambi

Tumepitisha majuma kadhaa tukitafakari kwa furaha jinsi ya kuishi kwa mpangilio unaoendana na sababu yetu ya kuweko.  Sasa tunageukia upande mwingine, kuangalia sura tofauti.  Picha ya Padre Donald Doll ya kijiji kilichopigwa mabomu huko Bosnia inaweza kutuashiria uovu wa uasi unaosababishwa na kumkana Mungu na pia nia mzuri ya Mungu kwa wanadamu wote.

Tunaelekea huko juma hili kwa kuwa tunataka kuona na kuonja maana hasa ya dhambi kama uasi wa kutisha dhidi ya Mungu.  Hii siyo kuangalia bila uyakinifu hali ya uovu wa kijamii tu bila uwajibikaji wa wahalifu.  Nia yetu ni kuitumia wiki hii katika kupata fahamu ya utambuzi wa kiburi kisicho na maana na kukuouna kufedheheshwa kwa Mungu na upinzani wa binadamu dhidi ya fadhili zake kwa dunia.  Kwa nini tunafanya hivi?  Tunafanya hivi kwa sababu ni mara chache tunauangalia uovu usoni, na kwa sasa tunapofanya hivyo ili tuweze kujua kwa undani zaidi upendo na huruma ya mungu, katika kifo na ufufuko wa mwanaye Yesu Kristu kwa ajili ya kutukomboa kutoka dhambi ya dunia.

Kwa hiyo kuna sura mbili katika juma hili:
1. Ile inayotujia juma hili ikionyesha dhambi za dunia
2. Sura ya Yesu juu ya Msalaba, akitukomboa kutoka katika dhambi na vitisho vya mauti.

Adui wa uhusiano wetu na Mungu hupenda kujificha asionekane nasi akihofia tunaweza kupata busara zaidi katika kujua maana hasa ya dhambi.  Kimsingi hii haihusu dhambi zetu binafsi, japokuwa sisi sote tu wadhambi.  Tunachotaka juma hili ni kukomaa zaidi kiroho na kuwa na hisia sahihi ya dhambi, dhana ambayo sehemu kubwa ya jamii yetu imeipoteza.

Mara kadhaa katika juma hili, tutatazama nyuma katika historia yetu na kuunda picha kutumia uwezo wetu wa kudhani — picha za vita na utumiaji mwingine wa mabavu, picha za kinyama, uvunjaji sheria, dhuluma, ukosaji nidhamu, ubadhilifu, ufisadi, uchoyo na kugomambania madaraka. Hayo vyote yanaonyesha jinsi binadamu tunavyoasi mapenzi ya Mungu astahiliye kusifiwa, kutukuzwa na binadamu ambaye anapaswa kutumia viumbe vingine vyote katika kufikia lengo hilo.

Ni kiasi gani cha unyimaji wa haki ya Mungu ya kusifiwa, kutukuzwa na tutumikiwa tunaweza kushuhudia juma hili?  Ni kiasi gani tutashuhudia ibada kwa miungu wa uwongo kama utajiri, utwana na madaraka? Kiasi gani cha ukosefu wa heshima kwa maisha ya binadamu tutashuhudia?  Na tena, ni kiasi gani cha ulaghai, uvunjaji wa sheria halali na ukiukwaji wa haki za binadamu utakuwa bayana mbele za macho yetu?  Tunataka kushuhudia ukubwa, mapana na marefu ya dhambiya dunia, ili kwamba tusisisite wala kutishika katika kutafakari athari zake.

Lengo letu si kuhukumu wala kuwa na hasira juu ya watendao dhambi.  Tunataka tu kushuhudia namna ambayo dhambi inawakilisha ukosefu wa shukrani kwa Mungu na kiburi kitupavyo uhuru bandia wa kumkana Mungu.
Kila siku katika juma hili utambuzi wetu wa uovu utakuwa ukiongezeka kiasi cha kuwa usiovumilika bila kuwa na utambuzi wa pili — utambuzi wa Mungu apokeaye yote kwa upendo na huruma.  Malipo kwa maovu yote na dhambi yapo katika mwili na damu ya Yesu Kristu anapokubali kufa pale msalabani.  Kifo chake ni bei ya yote yanayopotezwa na kupotoshwa na dhambi za binadamu.

Kila siku tunaifunga kwa shukrani zinazoongezeka kwa kadiri tunavyozidi kushuhudia wingi wa Rehema za Mungu.
Zana za Kukusaidia Kuanza Juma Hili

Hili ni juma muhususi kuona maendeleo yetu katika mafungo haya.  Mazoezi haya yamejengwa kufuatana na neema tulizopata katika majuma yaliyopita, kama jinsi ambavyo majuma yafuatayo yatakavyojengwa kufuatana na na neema za juma hili.  Katika juma hili tutakuwa tukitafakari juu ya mambo halisi ambayo kwa kawaida hatujishughulishi kuyatafakari.  Hapa pana ushauri halisi wa kulifanya juma hili liwe lenye mafanikio zaidi.

Kuwa makini jinsi unavyoianza na unavyoifunga kila siku.  Hii inakuwa chombo cha kutuweka tusipoteze lengo letu kirahisi, bali kubaki katika njia inayotakiwa kila siku.  Tunapoamka kila asubuhi na kujiandaa kwa shughuli za siku, tutenge muda mfupi tu wa kujikumbusha neema ambazo tungependa kujaliwa siku hiyo: kuingia ndani zaidi katika kujua maana hasa ya dhambi.  Hapa naweza kusali, kwa mfano, “Mungu, nipe nafasi ya kushuhudia na kupata hisia za ukatili wa uovu ambao unaonekana kutawala ulimwengu wetu.  Bwana, ningependa pia kuguswa na upendo na huruma yako isiyo na kipimo.”  Mwisho wa kila siku, naiacha sura ya Kristu msalabani ichukue nafasi ya yote yaliyojaza akili na moyo wangu katika siku.  Najaribu kuifanya picha hii ionekane katika uhalisi wake.  Pengine najaribu kujidhania naangalia juu msalabani kutazama uso wa Kristu Msulubiwa na kuzungumza naye nikimpa shukrani zangu.  Labda pia kuzungumza na Krisu Mfufuka uso kwa uso na kumwomba anionyeshe matundu au makovu ya misumari katika mikono yake, miguuni mwake na ubavuni mwake; makovu yaliyobaki kama ushuhuda kwetu wa upendo mkuu wa Mungu.

Yaliyomo katika juma hili yatahitaji juhudi zetu kubwa sanai, ila matunda tunayotegemea yanastastahilisha juhudi hii.  Picha za maovu, kwa mfano yaliotendeka katika mauaji ya Bosnia na Rwanda yanaweza kuwa milango wa kuingia katika hali ya kushushudia jinsi maovu ya ulimwengu wetu yanavyotisha.  Najaribu kufikiri kuhusu vita vyote katika historia na ukatili unaosababishwa kwa ajili ya kiongozi Fulani au kwa ajili ya tamaa ya madaraka tu.  Nawawaza watoto wasio na hatia ambao wanakua katika hali ya kunyimwa hata nafasi ya kushuhudia uhuru na hadhi ya utu.  Nawaza juu ya mifumo ya ufisadi na mizigo inayosababishwa nayo kwa binadamu wote.  Nawakumbuka marafiki wapendwa wangu wote ambao ni wahanga wa dhambi.  Labda ninashuhudia majonzi ya mtunzaji familia ashindwaye kupenda au uasi na yule anayeaminika na kupenda.

Ni vipi utambuzi wa huzuni hii, au hata vitendo vya kikatili tunaweza kuviweka moyoni vitawale mitazamo yetu ya maisha juma hili bila kuathiri amani mioyoni mwetu au utendaji wa kazi au mahusiano katika familia?  Hakika hatupendi zoezi hili liadhiri mioyo yetu.  Tunapenda kuondoa vyote vinavyotupofusha ili tuweze kuona na kuhisi nguvu za uovu kwa uhakika.  Hata hivyo wakati huo huo, tunataka kushuhudia nguvu ya Mungu anayetujali.  Juma hili lisiwe la kutukatisha tamaa, bali la kutupa matumaini.

Juma hili litakuwa neema kuu iwapo tutatunza kwa uaminifu na uangalifu mtazamo unaotegemewa: kumwomba Mungu neema ya kushuhudia jinsi dhambi ya ulimwengu ilivyo uovu na uasi dhidi ya Mungu; na kwa upande mwingine wingi wa rehema za Mungu zinazowekwa wazi katika kifo cha Yesu kwa ondoleo la dhambi ya dunia.
Kuziweka neema zinazopokelewa katika maandishi, kuwashirikisha wengine neema hizo, kuwatumia wengine habari za neema ulizopekea kwa barua pepe, au kuziandika katika mtandao huu ili zisomwe na wengine ni njia ya hakika ya kuingia ndani zaidi katika kuzishuhudia neema hizi na kisima chake kisichokauka, ndiye Mungu aliye na huruma sana.
Labda katikati ya wiki tunaweza kuchunguza maendeleo yetu.  Tunaweza kujiuliza: “Je! ni rahisi kwangu kuchunguza uovu wa dhambi za ulimwengu? Ni sawa kughadhibishwa nayo?  Ni vigumu kuongeza shukrani zangu kwa Mungu kwa ajili ya huruma yake?”

Kwa Ajili ya Safari: Kutafakari Dhambi
Tunapoanza kutafakari dhambi, iwe yetu au ile ya ulimwengu kwa kawaida kitendo hiki hakituletei furaha.  Kama mtu mmoja alivyosema, “hakuna chochote cha asili kuhusu dhambi”, hakika hakuna yeyote mwenye ambaye kwa asili hufurahia uharibifu wowote, uwe wa dhoruba au wa vita.  Kwa kadiri tunazidi kuwa watu wenye hisia nyepesi, ndivyo kadiri tunavyotishika katika kutazama au kuwaza juu ya ubovu wa vurugu na chuki.

Tutafakaripo kuhusu dhambi katika Mazoezi ya Kiroho, swali linalotawala ni iwapo hatia ni neema au kupotoka.  Labda naweza pia kuliweka swali hilo hivi: Je! fremu ya picha huiongezea picha chochote?  Hakika fremu huyaongoza macho kwenye kile inachokizingia.  Tunapofikiria juu ya uasi na ukosefu wa shukrani unaodhihirishwa katika dhambi, kipi ni picha na kipi ni fremu ya picha?

Kwa wengi wetu, kushiriki katika kutenda dhambi ya ulimwengu na kutenda dhambi binafsi haviachi nafasi ya jingine lolote, hivyo kwamba fremu inakuwa upendo wa Yesu unaokosa mantiki katika ulimwengu na kwetu binafsi kadhalika; kinyume cha hayo kinakuwa kweli tunapotafakari haya katika Mazoezi ya Kiroho.  Picha ya kati katika Mazoezi ya Kiroho daima ni upendo wa Kristu Yesu, kwetu na kwa ulimwengu mzima.  Kile kinachoonyesha kinaganaga upendo huu ni ukweli kuwa kila mara tunakataa na kupinga kuishi katika matumaini na mapendo.  Dhambi yetu ni sababu ya Yesu kuja na kuchukua nafasi ya kati katika fremu yote ya historia

Baba yangu alikuwa mwanasheria katika taasisi ya sheria ambayo mwito wao ulikuuwa “Mtu asiye na wakili ni jeraha baya kupita kiasi.”  Dhambi kubwa sana kwetu ni zile tunazozificha sisi wenyewe, tunakataa kumtambua na kumruhusu Yesu kuzibeba katika msalaba wake.  Yeye ni zaidi ya wakili kwetu—baada ya kubeba dhambi zetu, hatuachi wapweke bali kwa upendo mkuu, hukaa nasi katika dunia anayoipenda na huwa mponyaji wa majeraha yanayosababishwa na dhambi.

Kuna neema maalumu ya hatia inabobaki kuwa fremu na kutuongoza katika kujali halafu kupokea msamaha wa Yesu unaotuweka huru. Dhambi ni upotofu unaotuvuruga akili na kutuweka katika kitovu cha kutosamehewa.  Tunaweza kuyazungusha magurudumu yetu ya kiroho katika uchafu na matope yatukwamishayo na kutuongoza katika kujiteketeza nafsi, na katika kufanya hivyo tuna imani bandia kuwa Mungu ataona adhabu tunayojishurutishia na katika kufanya hivyo tunajiwekea matumamaini hadaa kuwa Mungu hatafanya lolote ila kutuonea huruma tu.  Hii haimweki Mungu kati ila nje ya fremu ya maisha yetu.  Mungu si mtazamaji mshabiki wala si mhakiki wa kazi za usanii.  Mungu ni mshiriki mtendaji katika maisha yetu.

Mazoezi ya Kiroho yanatukaribisha katika uhuru wa kumwacha Mungu awe Mungu na kujiweka wazi kupendwa siyo tu kama tulivyo sasa, bali pia kama tutakavyokuwa muda ujao.  Katika kusali juma hili, tunaweza kuwa wakweli bila kuwa wakanaji?

Katika Maneno Haya au Mengine Yanayofanana Nayo...

Bwana Wangu Mpendwa,

Nimechanganyikiwa: katika majuma manne yaliyopita, nimekuwa nikitafakari sura hizi za kupendeza—picha ya mama, ya mototo, ya mandhari ya kupendeza na watu wenye furaha; na katika sala zangu nimekuwa nikihisi mapendo na ulinganifu mtamu.  Lakini katika juma hili naona kijiji kilichopigwa mabomu na kuharibiwa na vita—picha ambayo inakera ulinganifu wa picha zilizotangulia.  Najua wazi kuwa upo katika upendo na ulinganifu.  Je! upo pia katika shari na uharibufu?

Inakuwa vingumu kwangu kusali nikiiangalia picha hiyo ya uharibifu.  Nataka kuwaombea watu ambao wamepoteza jamaa zao na makazi yao, ambao maisha yao yamebadilishwa na uharibifu huu wa kikatilii.  Napendelea watu hao waungwe mkono na wewe ili kupata amani wanayoikosa kutoka kwa wanadamu, amani katika maisha yao yaliyovunjwavunjwa kabisa..

Lakini tena ninapoingalia picha hiyo, nawawaza wale ambao wamejitenga nawe kiasi cha kusababisha uharibifu huu dhidi ya wanadamu wenzao.  Ni nini kinachotusukuma sisi wanadamu kutendeana vibaya kiasi hiki?  Unatuchukuliaje Ee Mungu unapotuangalia na kutuona sisi viumbe vyako tumapotendeana mabaya kiasi hicho?
Nafikiri kuhusu famila yangu na jinsi ninavyojihisi ninapotumia muda mwingi nikitayarisha zawadi kwa binti yangu—jinsi itakavyomfanya afurahi na kuridhika. Itakuwaje iwapo ataiangalia zawadi hiyo na kusema “asante” kisha akaitupia kabatini?  Hii itanifanya nijisikieje?  Najaribu kufikiri ni ufidhuli kiasi gani tunaokufanyia Mungu wetu tunapotenda mambo kama hayo unapotujalia zawadi kubwa ya maisha?

Nisaidie juma hili kuhisi jinsi ambavyo dhambi ni kukukana Mungu wetu na kuutupa upendo wako.  Nijalie juma hili nivishinde vyote vinavyoniogopesha kutazama na kutafakari vyote vilivyo na uovu duniani.  Nifumbue macho na moyo nione na kutambua jinsi ambavyo dhambi si lolote ila ukosaji wa shukrani kwako wewe uumbaye maisha, kutuzawadia sisi na kuyapa maana na mwelekeo.  Nataka kutokupendezwa na uovu namna nisivyotaka chochote kinachoniumiza kinisibu.  Nataka kuwa na silika ya kuhisi jinsi ubinafsi unavyovuruga na kuharibu nia na mpango wako mwema kwa ajili yetu viumbe vyako.

Ninapokuangali msalabani, nijalie kuhisi na kutambua jinsi ulivyojitwika na kutuondolea uovu wetu wote.  Nikushukuruje Bwana Wangu?  Nijalie nisidharau jinsi hisani na upendo  wako kwetu pale msalabani unatukomboa kutoka katika udhalimu na uharibifu wa dhambi na mauti.

Maandiko Matakatifu:

Wakolosai 2:9–15
Zaburi 10 and 73
1 Yohana 1:5–2:2
Luka 15:1–10

MAFUNGO YA KIROHO KUPITIA MTANDAO