Jinsi ya Kutumia Mtandao Huu Kufanya Mafungo

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara (FAQ).

Inawezekana vipi kufanya mafungo (ritriti) kwa mtandao? Mafungo ni KUTOKA KATIKA utaratibu wetu wa kawaida na pia ni KUINGIA KATIKA “sehemu” ambapo tunaweza kuzipokea vema zaidi neema ambazo Mungu anapenda kutupa.  Mafungo haya ya mtandao yanatupa nafasi kutazama mtandao huu kila juma na kupata mwongozo wa KUTOKA na KUINGIA.  Wengine kati yetu wana kompyuta zenye mtandao nyumbani na kazini.  Wengine inabidi waende kwa marafiki kusaidiwa au sehemu ambapo wanapata huduma hii kwa kulipia.  Inawezekana kupunguza gharama na muda kwa kwa kufungua mtandao huu na kuchapa kurasa za miongozo ya mafungo, na kuipitia juma moja baada ya jingine kufuatana na utaratibu.  Cha maana ni kutumia mwongozo wa juma moja katika juma linalohusika, kwa mfano kututumia mwongozo wa juma la kwanza katika wiki ya kwanza, na wala si miongozo ya juma la kwanza na la pili katika juma la kwanza la mafungo.  Baada ya kuanza mafungo, hutakiwi kupitia miongozo ya kanuma yajayo kabla ya kuyafikia.  Ni vema huwa makini katika kufuata utaratibu huu, kwa kuwa majuma yamepangwa katika hali ambayo juma la pili halina yaliyokuwemo katika juma la kwanza, ila linaanzia pale la kwanza lilipoishia.
Ni utaratibu gani nijizoeze kuufuata?

Kupata faida kubwa ZAIDI ya kiroho kupitia mafungo haya tutatumia mbinu au mazoezi matatu:

  • kusoma MWONGOZO wa JUMA HUSIKA kila tunapoanza juma hilo.
  • kutumia muda mfupi kusali KILA SIKU.
  • kupitia neema tulizojaliwa KILA WIKI; kuchangia neema tulizopata na mwongozi wa kiroho au wenzetu wafanyao mafungo haya (hili si sharti).
Je, mafungo haya ni kama kufanya Mazoezi ya Kiroho ya Mtakatifu Inyasi wa Loyola? Mafungo ya Siku Thelathini ya Mtakatifu Inyasi au Mazoezi ya Kiroho ya Mtakatifu Inyasi wa Loyola yanategemewa kufanywa na mfungaji mmoja kuwa na mwongozi wake wa mafungo, ambapo mfungaji hutenga muda wa siku 30 za ukimya wa maombi, tafakari ya Neno la Mungu na ya maisha yake, na taamuli. Katika kipindi hicho mfungaji hujitenga na maisha ya shughuli za kawaida za kila siku.  Kiini cha Mazoezi ya Kiroho ya Mtakatifu wa Loyola ambacho ni kukua katika uhusiano wetu na Mungu na kuwa na uhuru zaidi wa kiroho, ndivyo vinavyohamasisha mafungo haya na utaratibu wake, kutuwezesha wengi wetu kufaidi matunda ya kiroho ya mazoezi hayo.
Itakuwaje kama mimi sijawahi kufanya mafungo yoyote? Hilo si tatizo.  Mafungo haya yamewekwa katika utaratibu ambao ni RAHISI KUFUATA.  Kilicho muhimu ni kukumbuka kuwa Mungu hahitaji mengi kutoka kwetu ili kutupa baraka na neema zake nyingi.  Mafungo haya yanatoa mapendekezo ya sala katika juma zima—mapendelezo ambayo humsaidia mfungaji kupata mwanga wa neema zipi hasa anazotaka kumwomba Mungu, na kujiumbia moyo ulio tayari kupokea neema hizo.  KILICHO KIZURI ZAIDI ni kuwa tunafanya mafungo haya katika mazingira ya maisha yetu ya kila siku, hivyo basi kuyaneemesha na kuyapa maana zaidi maisha hayo huku nasi tukishuhudia.  Kwa maneno mengine tunamshuhudia Mungu akiishi nasi na kushiriki katika yote tufanyayo na tufanyiwayo kila siku.
Naogopa siku zingine naweza nisipate muda wa “sala”.

Suala hili ni rahisi kuliku tunavyodhani.  Jaribu kuwa na mtazamo wa mafungo haya kama kitu kitu cha thamani TUNACHOJIZAWADIA.  Tuamini kuwa mafungo haya hayatupotezei muda ila ni mojawapo ya namna nzuri na za busara za kuutumia muda wetu.  Hii itafanya yote kuwa rahisi kwa kuwa kwa asili yetu tunapenda kutenda mambo yanayotupendeza na yaliyo na faida na maana.

Tunaweza kuanza kwa kujitengea dakika 10 hadi 15 kila siku katija majuma ya au miezi ya mwanzoni.  Yawezekeana muda mzuri zaidi wa sala ukajitokeza kwetu kwa kujaribu kwanza nyakati mbalimbali:  asubuhi kabla ya kwenda kuanza shughuli za kila siku, muda wa mapumziko ya mchana, jioni baada ya kazi, muda kabla ya kulala, nk.

Kumbuka kuwa Mwongozo wa mafungo wa wiki husika utakuwa ukikupa ushauri na kukusaidia kufanya mafungo.
Waweza kusema nini kuhusu “hiari” ya kuzungumza na kuchangia na mwongozi wa kiroho au na kikundi cha wenzangu?

Kila mmoja wetu afanyaye mafungo haya kwa mtandao atakuwa akifanya UKAGUZI wa kula juma lake la mafungo kuona jinsi siku moja ilivyohusiana na nyingine, neema alizopokea, alama za uwepo wa Mungu katika maisha yake, nk.  Hii hufanya juma kuwa kitu kimoja katika maisha ya afanyaye mafungo, kama vile tofali moja katika matofali 34 yajengayo nyumba yake ya mafungo.  Baadhi ya MATUNDA ya mafungo yatajitokeza pale tunapokuwa na utambuzi kuwa kuna mwelekeo fulani chanya pale tunapoweka katika mtiririko mmoja hisia zetu za ndani, matukio na zawadi mbalimbali za Mungu.  Hii hutuwezesha kuona na kushuhudia jinsi Mungu alivyokuwa na anavyokuwa pamoja nasi katika maisha yetu.Kuzungumza na mwongozi wa kiroho kuhusu maendeleo yetu katika hii safari yetu ya kiroho ya kila juma ni utaratibu mzuri sana wa kujiwajibisha na vilevile kufaidika na neema ambazo tumepokea. 

Mwongozi wa kiroho aweza kuwa yule tuliyenaye au tutakayemwomba aambatane nasi katika mafungo haya.  Mwongozi wa kiroho hutusaidia kuchanganua yale yatendekayo katika safari yetu ya mafungo hivyo kwamba tunaweza kirahisi zaidi kutambua mguso au mwito wa Mungu.  Mwongozi wa kiroho pia hutoa msaada na mwongozo.  Kikundi cha kuchangia chaweza kuwa chama cha kitume ambacho sisi tayari ni wanachama au pia kikundi tulichounda ili kufanya mafungo haya pamoja.  Ni vizuri kwa wale wanaofanya mafungo pamoja kukutana mara mbili kwa mwezi, na ni vema kuanza pamoja na kuendelea pamoja juma kwa juma. 

Katika kuchangia katika kikundi tunaweza kugundua neema tulizopewa na Mungu katika juma ambazo hatukuwa tumezitambua — hii hutujaza moyo wa shukrani kwa Mungu na kutupa hamasa ya kuendelea na mafungo.  Tunapokutana kika mmoja huelezea kwa kifupi yale yanayoendelea katika mafungo yake, hasahasa yanayogusa moyo wake, mabadiliko anayoona katika maisha yake na neema anazoshuhudia kuzipokea tangu wakutane mara ya mwisho.  Kwa msaada zaidi soma malezo katika ukurasa wetu wa usaidizi wa kufanya mafungo haya katika kikundi.

Tutegemee nini baada ya kufanya mafungo haya ya kiroho kwa mtandao?

Rehema za Mungu zapita uwezo wa akili zetu na ukarimu wake kwetu hauna mfano.  Hii ni kusema hatuna uwezo kamili wa kuelezea zawadi zake kwetu tunapomfunulia mioyo yetu.  Tunachoweza kusema kwa uhakika wa uelewefu wetu ni kuwa katika mafungo haya ya kiroho tunakua katika uhusiano wetu na Mungu.  Neema nyingine ambazo ni bayanani kukua katika amani ya moyoni itokanayo na kuwa na utambuzi wa kina jinsi Mungu anavyotupenda.  Zaidi tunakuwa na uhuru zaidi wa kiroho kwa kuwa Mungu anatuondolea vizuizi vingi vilivyokuuwa vinatudororesha katika kumpenda yeye na kuwapenda.  Hapa basi tunajengewa moyo wa ujasiri wa kukabiliana na na matatizo mengi ya maisha bila kukata tamaa wala kushawishika kumkana Mungu.  Kwa yote hayo, ni wazi kuwa hatukosei tukitumaini kuwa mwisho wa mafungo haya tutakuwa na hamasa zaidi kusaidia wenzetu katika magumu ya hapa duniani.


 
Kurudi kwenye
MAFUNGO KUPITIA MTANDAO
Kurasa Mama—Home Page.
Helps for
making this retreat
on your own.
Helps for
a group
making this retreat.